MATAJIRI (points)

MATAJIRI (points)

MINBOOKLET

MINBOOKLET

SHUKRANI

SHUKRANI

Wednesday, August 31, 2016


IK5 anaongoza kwa kura 2, kwani amebahatika kupata Kura ya bahati, endapo kuanzia Leo 31/08/2016 hadi tar 31/10/2016 hatajitokeza yeyote katika washiriki 49 >>>KUPIGA/KUPIGIWA KURA, basi IK5 atashinda 1,000,000/=,

Sunday, August 14, 2016

Ni Charles Gerald kutoka Mount Meru mwenye Kura nyingi kundi la 10, hivyo ndiye mshindi kwa Kura 572, huku aliyemfuatia nafasi ya pili ni kutoka UDOM akiwa amepata kura 541. Tukumbuke kuwa jumla yapo makundi 10 msimu huu wa 4, na hili ndilo kundi la 10 la mwisho.
Wote kundi hili wameingia hatua ya pili ya Kura za thamani

Thursday, August 11, 2016

Lilikuwa kundi la 9 ambalo Emma alishiriki na kuweza kufika hatua ya ushindi kwa kura 472, akitokea SAUT - Arusha, Mshindi wa pili katika kundi  hili ametokea UDSM, washiriki wote kundi hili wameingia hatua ya 2 ya Kura za thamani.

Wednesday, August 10, 2016

Aman Hamis ni mshindi wa kundi la 8, Msimu wa 4. Ni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) amepata Kura 514. 
Washiriki wote katika kundi lake wameingia hatua ya pili ya kura za thamani.

Friday, July 22, 2016

Glory ni mshindi wa kundi la 7 kutoka Chuo cha Ushirika kilichopo Moshi  (MOCU), idadi ya Kura zake ni 418 huku mshiriki kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishika nafasi ya pili katika kundi.
Washiriki wote wamefanikiwa kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi hupata Tsh 1,000,000/= (Milioni moja).

Thursday, July 21, 2016

JOHNAS CAMILLIUS ni kijana aliyemaliza kidato cha sita kutoka MINAKI HIGH SCHOOL,  alishiriki Mwitiko Binafsi kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kufanikiwa kuibuka mshindi wa kundi, huku nafasi ya pili ikishikwa na WINFRIED MGAYA  a.k.a KING BOZ (The musician Boy) kutoka MUHAS
Kundi zima la 6 wameweza kuingia hatua ya pili ya  Kura za thamani. 
Kura 511 zilimfanikisha Suzan Laiser kuongoza kundi la 7 hivyo kuwa mshindi wa kundi, Ameshiriki kutoka  CHUO CHA IRINGA.
Washiriki  wa kundi lake wote wamefuzu kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi katika hatua hii ya pili hupata Tsh Milioni moja (1,000,000/=).

Wednesday, July 13, 2016

Ni kijana John kutoka St. Joseph, amekuwa ndiye mshindi kwa kupigiwa kura nyingi kutoka kwa watu mbalimbali toka pande za nchi ya TANZANIA pia baadhi kutoka nchi za Ng'ambo
Kwa ujumla WASHIRIKI wote kutoka kundi lake wameingia hatua ya pili ya Kura za thamani zitakazoanza Mara baada ya makundi yote 10 kumalizika.

Wednesday, July 6, 2016

Huyu ni mrembo NELLY, msichana ambaye amewakilisha vema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa kura nyingi zipatazo 382. 
Nafasi ya pili katika kundi hili la 3 imemwangukia msichana kutoka SAUT (Arusha Campus) 
Washiriki wote ndani ya kundi la 3, wameweza kuingia hatua ya pili ya kura za thamani, zitakazoanza kupigwa mara baada ya kukamilika makundi yote kumi (10).

Tuesday, June 21, 2016

Huyu ni kijana aliyeshiriki kundi la pili MSIMU WA 4, kutoka UDSM, namba yake ya utambulisho kwenye kundi lake ilikuwa #1, ambapo aliweza kuongoza kundi lake kwa kura 194
Kundi hili la pili wote wamefanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili ya kura za thamani, kuwania ushindi wa kiasi cha Tsh Milioni moja.

Anaitwa Vidah Msigwa ambaye ameweza kushinda kwa kura nyingi kwenye kundi lake la 1 la msimu wa 4. Amewakilisha UDSM kwa kupata Kura 651 kwenye sanaa ya picha za matangazo kwa utambulisho #4. Nafasi ya pili kwenye kundi hili imeshikiliwa na Johnia kutoka UDSM aliyeshiriki akiwa na namba 3 ya utambulisho kwenye kundi, amefanikiwa kupata jumla ya kura 438.
Hivyo washiriki wote wa kundi hili wamevuka kuingia hatua ya pili itakayoshirikisha makundi 10 yenye jumla ya WASHIRIKI 50 kuweza kupigiwa kura za thamani ili mshindi mwenye kura nyingi aibuke na kiasi cha Tsh 1,000,000/= (Milioni moja).


Wednesday, March 9, 2016

Ni mshiriki kundi la 10, Anaitwa Jackline kutoka Sjmc-Udsm
Ameweza kupata Kura nyingi zaidi, Hivyo yeye ni mshindi Wa
Kundi hili la 10.
Washiriki wote Wa kundi hili wameingia HATUA ya pili ya Kura za thamania, ambapo mwenye Kura nyingi ataibuka na ushindi wa Tsh 1,000,000/= .... Jumla ya washiriki wote ni 50 watakaokuwemo kwenye ushindani wa Kura za thamani.

Wednesday, March 2, 2016

Daniel ni ni mshiriki Wa kundi la 9, hili ni kundi la mwisho kwa
Upande wa wavulana MSIMU HUU WA TATU
Kundi hili la 9 wote wamefanikiwa kuingia hatua ya pili ya kura za thamani, atakayepata Kura nyingi ataibuka na ushindi Wa kiasi cha Tsh 1,000,000/=
Jumla ya makundi; YAPO KUMI (10)
Jumla ya washiriki; WAPO HAMSINI (50)

Tuesday, February 23, 2016

Kundi la nane lilikuwa na washiriki watano, ambapo wanne ni wa Sjmc-Udsm pia mmoja ni wa Coss-Udsm. Ritha kutoka Sjmc-Udsm, ndiye mshindi wa kundi hili kwa kura 201. Lakini wote wameingia hatua ya pili ya ushiriki wa kurĂ  za thamani ambapo mshindi mwenye kura nyingi hushinda kiasi cha Shilingi Milioni Moja (Tsh 1,000,000/=).

Wednesday, February 17, 2016

Ephrem alidhihirisha kukubalika na walio wengi kwa kupigiwa Kura nyingi zaidi. Kundi lake lilinadiwa kama kundi la Ronaldo kutokana na VIJANA wote kuwa na vipaji vya picha za mnato kwa uwezo wa hali ya juu. Alipata Kura 234 huku mpinzani wake wa karibu akimkabili kwa kura 122.
Wote katika kundi hili wameingia hatua ya pili ya kinyang'anyiro cha Shilingi 1,000,000/=.

Wednesday, February 10, 2016

Mary ni MSHINDI kwa kura 182, ambapo namba yake ya utambulisho katika kupigiwa Kura ilikuwa No. 3,  Ni mshiriki wa kundi la sita na ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu (SJMC-UDSM).
Kundi lake limefanikiwa pia kuingia HATUA ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi kati ya washiriki 50, ataibuka na ushindi wa kiasi cha Tsh 1,000,000/=.

Tuesday, February 2, 2016

Ni kijana kutoka Sjmc-Udsm, Ameweza kuibuka
mshindi kwa kura nyingi baada ya kupigiwa na wadau wengi
Kuwa ana uwezo kwenye kipaji cha MATANGAZO YATUMIAYO
PICHA ZA MNATO. Kundi lake kwa ujumla linaingia hatua ya pili ya kura zenye thamani ili kumpata mshindi atakayemiliki kitita cha Shilingi Milioni Moja (1,000,000/=) za Kitanzania. Hatua hii ya pili itawashirikisha washiriki 50 ambao wanatokana na makundi kumi (10) ya MSIMU WA TATU.

Wednesday, January 27, 2016

Kwa jina anaitwa AIKA, mshiriki wa kundi la nne
Ambapo baada ya kuhesabiwa Kura zake ilithibitishwa 
kuwa ameongoza kwa kura nyingi, HATUA YA PILI
YA KURA ZA THAMANI INAKUJA, AMBAPO MSHINDI 
WA KURA NYINGI HUSHINDA KIASI CHA TSH, MILIONI
MOJA (1,000,000/=). washiriki wote wa kundi la nne 
wataunganishwa wote katika hatua hii ya pili ya kura
za thamani.