MATAJIRI (points)

MATAJIRI (points)

MINBOOKLET

MINBOOKLET

SHUKRANI

SHUKRANI

Friday, July 22, 2016

Glory ni mshindi wa kundi la 7 kutoka Chuo cha Ushirika kilichopo Moshi  (MOCU), idadi ya Kura zake ni 418 huku mshiriki kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishika nafasi ya pili katika kundi.
Washiriki wote wamefanikiwa kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi hupata Tsh 1,000,000/= (Milioni moja).

Thursday, July 21, 2016

JOHNAS CAMILLIUS ni kijana aliyemaliza kidato cha sita kutoka MINAKI HIGH SCHOOL,  alishiriki Mwitiko Binafsi kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kufanikiwa kuibuka mshindi wa kundi, huku nafasi ya pili ikishikwa na WINFRIED MGAYA  a.k.a KING BOZ (The musician Boy) kutoka MUHAS
Kundi zima la 6 wameweza kuingia hatua ya pili ya  Kura za thamani. 
Kura 511 zilimfanikisha Suzan Laiser kuongoza kundi la 7 hivyo kuwa mshindi wa kundi, Ameshiriki kutoka  CHUO CHA IRINGA.
Washiriki  wa kundi lake wote wamefuzu kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi katika hatua hii ya pili hupata Tsh Milioni moja (1,000,000/=).

Wednesday, July 13, 2016

Ni kijana John kutoka St. Joseph, amekuwa ndiye mshindi kwa kupigiwa kura nyingi kutoka kwa watu mbalimbali toka pande za nchi ya TANZANIA pia baadhi kutoka nchi za Ng'ambo
Kwa ujumla WASHIRIKI wote kutoka kundi lake wameingia hatua ya pili ya Kura za thamani zitakazoanza Mara baada ya makundi yote 10 kumalizika.

Wednesday, July 6, 2016

Huyu ni mrembo NELLY, msichana ambaye amewakilisha vema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kuibuka na ushindi wa kura nyingi zipatazo 382. 
Nafasi ya pili katika kundi hili la 3 imemwangukia msichana kutoka SAUT (Arusha Campus) 
Washiriki wote ndani ya kundi la 3, wameweza kuingia hatua ya pili ya kura za thamani, zitakazoanza kupigwa mara baada ya kukamilika makundi yote kumi (10).

Tuesday, June 21, 2016

Huyu ni kijana aliyeshiriki kundi la pili MSIMU WA 4, kutoka UDSM, namba yake ya utambulisho kwenye kundi lake ilikuwa #1, ambapo aliweza kuongoza kundi lake kwa kura 194
Kundi hili la pili wote wamefanikiwa kuingia kwenye hatua ya pili ya kura za thamani, kuwania ushindi wa kiasi cha Tsh Milioni moja.

Anaitwa Vidah Msigwa ambaye ameweza kushinda kwa kura nyingi kwenye kundi lake la 1 la msimu wa 4. Amewakilisha UDSM kwa kupata Kura 651 kwenye sanaa ya picha za matangazo kwa utambulisho #4. Nafasi ya pili kwenye kundi hili imeshikiliwa na Johnia kutoka UDSM aliyeshiriki akiwa na namba 3 ya utambulisho kwenye kundi, amefanikiwa kupata jumla ya kura 438.
Hivyo washiriki wote wa kundi hili wamevuka kuingia hatua ya pili itakayoshirikisha makundi 10 yenye jumla ya WASHIRIKI 50 kuweza kupigiwa kura za thamani ili mshindi mwenye kura nyingi aibuke na kiasi cha Tsh 1,000,000/= (Milioni moja).


Wednesday, March 9, 2016

Ni mshiriki kundi la 10, Anaitwa Jackline kutoka Sjmc-Udsm
Ameweza kupata Kura nyingi zaidi, Hivyo yeye ni mshindi Wa
Kundi hili la 10.
Washiriki wote Wa kundi hili wameingia HATUA ya pili ya Kura za thamania, ambapo mwenye Kura nyingi ataibuka na ushindi wa Tsh 1,000,000/= .... Jumla ya washiriki wote ni 50 watakaokuwemo kwenye ushindani wa Kura za thamani.

Wednesday, March 2, 2016

Daniel ni ni mshiriki Wa kundi la 9, hili ni kundi la mwisho kwa
Upande wa wavulana MSIMU HUU WA TATU
Kundi hili la 9 wote wamefanikiwa kuingia hatua ya pili ya kura za thamani, atakayepata Kura nyingi ataibuka na ushindi Wa kiasi cha Tsh 1,000,000/=
Jumla ya makundi; YAPO KUMI (10)
Jumla ya washiriki; WAPO HAMSINI (50)

Tuesday, February 23, 2016

Kundi la nane lilikuwa na washiriki watano, ambapo wanne ni wa Sjmc-Udsm pia mmoja ni wa Coss-Udsm. Ritha kutoka Sjmc-Udsm, ndiye mshindi wa kundi hili kwa kura 201. Lakini wote wameingia hatua ya pili ya ushiriki wa kurĂ  za thamani ambapo mshindi mwenye kura nyingi hushinda kiasi cha Shilingi Milioni Moja (Tsh 1,000,000/=).