MATAJIRI (points)

MATAJIRI (points)

MINBOOKLET

MINBOOKLET

SHUKRANI

SHUKRANI

Monday, November 30, 2015

Mariam aliyekuwa na utambulisho wa 5G1
Ndiye MSHINDI wa kiasi cha Tsh 1,000,000/=
Kilichokuwa kimetengwa kwa washiriki 50
wa MWITIKO BINAFSI huku wakiwa na safari ndefu ya kushiriki, ikiwa ni pamoja na Photo of the week, 5Group Winner na hatimaye shindano la mwisho, lililojumuisha WASHIRIKI wote 50 kutoka makundi kumi (10), 

Leo 30/11/2015 tunashuhudia Mariam akifaulu kukusanya kura za thamani zilizofikia idadi ya 166 na kushinda milioni moja

Mariam pia alishinda taji la UDSM - PHITOJENIC No. 1

MSHINDI WA MWITIKO BINAFSI,  kiasi cha Tsh Milioni Moja sasa kutangazwa saa 12:00 jioni ya Leo TAR 30/11/2015

Sunday, November 29, 2015

Kura za thamani za 2G2 na 5G1
Leo ikiwa ni SIKU ya mwisho na mpishano wa kura ni KURA MOJA TU.
Mwisho Wa upigaji kura ni leo 29/11/2015 saa 23:59 juu ya alama.

Thursday, November 26, 2015


MWITIKO BINAFSI studio imefunguliwa, itafanikisha picha za mnato na utengenezaji wa matangazo yahusuyo picha. Pia itashughulika na mikataba ya watakaochaguliwa kwa ajili ya MATANGAZO YA KIBIASHARA YAHUSUYO/YANAYOHITAJI PICHA ZA MNATO/ MTEMBEO (VIDS). 
Ipo Mikocheni, School of Journalism road, Karibu na SJMC / MLIMANI TV.

Tuesday, November 24, 2015

SIKU zimebaki chache, hatujui MSHINDI atakuwa nani,
Je wewe unaonaje? Na je wao 2G2 na 5G1 wanaonaje?
KITENDAWILI KUTEGULIWA TAR 30/11/'15 ATAKAPOTANGAZWA MSHINDI MWENYE KURA NYINGI ZA THAMANI.

Saturday, November 21, 2015

Friday, November 20, 2015

Tar 20/11/2015 tunashuhudia 2G2 na 5G1 wakiwa wamefungana kwa kura, Je nani atashinda endapo nguvu ZAO za kupigiwa kura ni sawa?.

Tuesday, November 17, 2015

2G2 anaongoza kwa kura za thamani, Yupo kwenye list ya washindi kumi walioshinda kwenye makundi yao kwa kupigiwa kura, Endapo ataendelea kuongoza hadi tarehe 29/11/2015 Hadi muda wa saa 23:59, basi atatangazwa mshindi wa Tsh 1,000,000/= za Kitanzania.
5G1 ni Mshindi wa Photogenic No. 1, SJMC-UDSM,  2015-2016
Pia alishinda kundi lake la wasichana watano kwa kura za kupigiwa na watu mbali mbali.
Hatua ya sasa ni ya kura za thamani ambapo 5G1
Anashikilia nafasi ya PILI kuelekea USHINDI wa Tsh Milioni Moja.

Sunday, November 15, 2015

2G2 anaongoza kwa kura 7 zenye thamani, zina thamani kwa kuwa kura moja thamani yake ni Tsh 2000/=

2G2 ndiye aliyeongoza katika kundi lake ambalo lilikuwa la KWANZA kwa wavulana kushiriki katika kupigiwa kura ili waweze kuingia hatua hii kubwa ya kura za thamani.
Cha kushangaza katika kuhesabu kura zake ilibainika kuwa alimzidi mpinzani wake kwa kura 1 tu, hivyo kura zake zilihesabiwa mara saba ili kujiridhisha. Ifahamike kwamba washiriki katika kundi lake walikuwa watano (5) na mpinzani wake mwenye ushawishi kwa watu kutokana na sanaa yake ya muziki wa kizazi kipya alikuwa 2G1
Huyu ni 2G1 ambaye hivi karibuni imefanya collabo Kimziki na msanii mkubwa wa Nigeria ambaye ni D' Banj.
Hakika 2G1 alishangaa kuona kura moja tu, ikimdondosha katika kushinda kwenye kundi lake.

Wednesday, November 11, 2015

6G2, 5G4 na 9G2 walipata kura ya bahati kama ilivyooneshwa tarehe walizobahatika kupata kura. Ambapo 6G2 wa kundi la sita alipata kura yake tarehe 08/11/2015, Pia siku iliyofuata 5G4 alipata kura Tar 09/11/'15 na aliyefunga ukurasa wa kura za bahati ndiye 9G2 ambaye alipata kura yake ya bahati Tar 10/11/'15. Baada ya kura hizi za bahati, zinafuata kura za awamu ya PILI za kupigiwa/kujipigia na kiasi cha Tsh Milioni Moja kitatolewa kwa atakayeshinda ifikapo Tar 30/11/2015.

Tuesday, November 10, 2015

10G5 ni mshiriki kutoka kundi la 10 ambalo lilikuwa kundi la mwisho. Kura ya bahati 07/11/2015 inampa nafasi nzuri ya kusonga mbele katika ukusanyaji wa kura zaidi. 10G5 anaweza kushinda kiasi cha milioni moja endapo atakuwa na kura nyingi zaidi. 

Saturday, November 7, 2015

4G2 ni mshindani ndani ya kundi lililokuwa la wasichana, Namba 4  (The 4th GROUP) ,  Pia alikuwa tano bora ya wasichana waliofanya vema katika kipaji cha picha za mnato (PHOTO OF THE WEEK - SJMC) Tar. 06/11/2015 kura ya bahati imemdondokea na kumweka katika nafasi nzuri ya kuuelekea USHINDI wa kiasi cha Tsh 1,000,000/=.

Friday, November 6, 2015

7G5 Alishiriki katika kundi la wasichana watano na kuibuka mshindi kwa kura nyingi dhidi ya mwenzake kwa kupata kura nyingi zilizopigwa na watu mbali mbali kutoka nchini na nchi za nje. Tar 05/11/2015 amepata kura ya bahati inayompa nafasi nzuri ya mwanzo wa ushindi wa Tsh 1,000,000/= Endapo atapata kura nyingi zaidi kuliko washiriki mwenzake 49.
6G3 anatokea kundi namba sita, Ni mshindi aliyeshinda kundi lake la wasichana watano, Kwa sasa yu  miongoni mwa washiriki 50 kwenye hatua ya kushindania kiasi cha Tsh Milioni Moja (1,000,000/=).
7G4 ni mshiriki PHOTO OF THE WEEK, SJMC-UDSM,
Kundi lake la kura za kupigiwa na wadau lilikuwa namba saba.
Kura ya bahati kwake imemdondokea TAR 03/11/2015
Ikiwa ni hatua bora kwake kuweza kushinda milioni moja
endapo uwingi wa kura utakuwa zaidi ya mwenzake.

Thursday, November 5, 2015

4G1 ni miongoni mwa washiriki watano waliopigiwa kura MWITIKO BINAFSI, PHOTO OF THE WEEK, Sjmc-Udsm.
Ni wa kundi la wasichana ambalo lilikuwa la nne (4th GROUP)
Kura yake ya bahati kwa TAR. 02/11/2015, Ni mwanzo mzuri kwake katika ukusanyaji kura zaidi ili aweze kushinda 1,000,000/= Fedha taslimu za Kitanzania.
2G3 ni mshiriki mwenye kura ya bahati tar 01/11/2015, Alishiriki katika kupigiwa kura akiwa kundi la PILI lililokuwa na  wavulana watano, AMESHINDA PIA KUWA KIJANA NAMBARI MOJA KATIKA UWEZO WA NGUVU KIFASHENI (POWERFUL FASHION BOY) SJMC-UDSM, 2015/16. Kwa sasa yu katika ushindanivu wa kiasi cha Tsh Milioni Moja akiwa na washiriki mwenzake 49, Na atakayepata kura nyingi ndiye atakayekuwa mshindi. 

Wednesday, November 4, 2015

8G3 anatokea BOYS GROUP kundi la NANE la walioshiriki mchakato wa upigiwaji kura kutoka kwa watu mbali mbali nchini na nchi za nje. Kwa sasa ameingia katika hatua shindanivu zaidi yenye washiriki hamsini, Hivyo basi kura ya bahati aliyopata tar 31/10/2015 ni muhimu kwake kuuelekea USHINDI wa Tsh milioni moja (1,000,000/=) endapo ataibuka na kura nyingi kupita mwenzake 49.

Tuesday, November 3, 2015

Anatokea kundi la 10, ambalo lilikuwa kundi la mwisho katika kuhitimisha washiriki hamsini (50) wa mwitiko binafsi
Pia alishiriki upigiwaji kura kundi (10th BOYS GROUP) lililokuwa na washiriki watano (5) wavulana.
Kwa sasa 30/10/2015 amepata kura ya bahati inayompa nafasi nzuri ya kuuelekea ushindi wa kiasi cha Tsh milioni moja.

Sunday, November 1, 2015

8G2 alikuwa mshindi wa kundi NANE (Boy's Group)
Tar 29 / 10 / 2015  amebahatika kupata kura ya
bahati inayompa nguvu ya kuelekea ushindi wa kiasi cha shilingi milioni moja.