MATAJIRI (points)

MATAJIRI (points)

MINBOOKLET

MINBOOKLET

SHUKRANI

SHUKRANI

Wednesday, August 31, 2016


IK5 anaongoza kwa kura 2, kwani amebahatika kupata Kura ya bahati, endapo kuanzia Leo 31/08/2016 hadi tar 31/10/2016 hatajitokeza yeyote katika washiriki 49 >>>KUPIGA/KUPIGIWA KURA, basi IK5 atashinda 1,000,000/=,

Sunday, August 14, 2016

Ni Charles Gerald kutoka Mount Meru mwenye Kura nyingi kundi la 10, hivyo ndiye mshindi kwa Kura 572, huku aliyemfuatia nafasi ya pili ni kutoka UDOM akiwa amepata kura 541. Tukumbuke kuwa jumla yapo makundi 10 msimu huu wa 4, na hili ndilo kundi la 10 la mwisho.
Wote kundi hili wameingia hatua ya pili ya Kura za thamani

Thursday, August 11, 2016

Lilikuwa kundi la 9 ambalo Emma alishiriki na kuweza kufika hatua ya ushindi kwa kura 472, akitokea SAUT - Arusha, Mshindi wa pili katika kundi  hili ametokea UDSM, washiriki wote kundi hili wameingia hatua ya 2 ya Kura za thamani.

Wednesday, August 10, 2016

Aman Hamis ni mshindi wa kundi la 8, Msimu wa 4. Ni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDBS) amepata Kura 514. 
Washiriki wote katika kundi lake wameingia hatua ya pili ya kura za thamani.

Friday, July 22, 2016

Glory ni mshindi wa kundi la 7 kutoka Chuo cha Ushirika kilichopo Moshi  (MOCU), idadi ya Kura zake ni 418 huku mshiriki kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akishika nafasi ya pili katika kundi.
Washiriki wote wamefanikiwa kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi hupata Tsh 1,000,000/= (Milioni moja).

Thursday, July 21, 2016

JOHNAS CAMILLIUS ni kijana aliyemaliza kidato cha sita kutoka MINAKI HIGH SCHOOL,  alishiriki Mwitiko Binafsi kupitia Chuo Kikuu cha Dar es salaam na kufanikiwa kuibuka mshindi wa kundi, huku nafasi ya pili ikishikwa na WINFRIED MGAYA  a.k.a KING BOZ (The musician Boy) kutoka MUHAS
Kundi zima la 6 wameweza kuingia hatua ya pili ya  Kura za thamani. 
Kura 511 zilimfanikisha Suzan Laiser kuongoza kundi la 7 hivyo kuwa mshindi wa kundi, Ameshiriki kutoka  CHUO CHA IRINGA.
Washiriki  wa kundi lake wote wamefuzu kuingia hatua ya pili ya Kura za thamani ambapo mshindi katika hatua hii ya pili hupata Tsh Milioni moja (1,000,000/=).

Wednesday, July 13, 2016

Ni kijana John kutoka St. Joseph, amekuwa ndiye mshindi kwa kupigiwa kura nyingi kutoka kwa watu mbalimbali toka pande za nchi ya TANZANIA pia baadhi kutoka nchi za Ng'ambo
Kwa ujumla WASHIRIKI wote kutoka kundi lake wameingia hatua ya pili ya Kura za thamani zitakazoanza Mara baada ya makundi yote 10 kumalizika.